Muimbaji,
Prince alikuwa akitibiwa kutokana na kutumia madawa ya kulevya
kupitiliza siku sita kabla ya kifo chake, TMZ wameandika.
Kwa
mujibu wa tovuti hiyo, ndege binafsi ya Prince ilitua kwa dharura huko
Moline, Illinois Ijumaa iliyopita, saa chache baada ya kutumbuiza
Atlanta.
Kipindi
hicho wawakilishi wake walidai kuwa alikuwa akisumbuliwa na mafua, kitu
ambacho kilizua maswali kwasababu ndege yake ilikuwa imebakiza dakika
48 tu kufika nyumbani kabla ya kuamua kutua kwa dharura.
Vyanzo
mbalimbali kutoka Moline vimeuambia mtandao huo kuwa Prince aliwahishwa
hospitali na kupewe huduma ya haraka (save shot) kumsaidia.
Vyanzo
hivyo vimedai kuwa madaktari walimshauri Prince akae hospitali hapo kwa
saa 24. Watu wake walitaka chumba binafsi na walipoambiwa kuwa
haiwezekani, Prince na wenzake waligoma.
Muimbaji
huyo aliondoka saa tatu baada ya kufika hapo na kuelekea nyumbani.
Vyanzo hivyo vimedai kuwa Prince aliondoka akiwa hajisikii vizuri.
Prince alikutwa hajitambui jana kwenye lifti kabla ya kutangazwa kuwa amefariki.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment