Maua Saleh ‘Maua Sama’.
WAKALI wa sauti za kumtoa nyoka pangoni, Maua Saleh ‘Maua Sama’ pamoja na Hellen George ‘Ruby’ wanatarajiwa kukutana uso kwa uso na staa wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Smith ‘Ne-Yo’, katika bonge la shoo litakalofanyika Mei 21, mwaka huu ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Hellen George ‘Ruby’.
Akizungumza na Over Ze Weekend, mratibu wa shoo
hiyo inayotambulika kama Jembeka Festival 2016, Sebastian Ndege alisema
kuwa mbali na Maua na Ruby, usiku huo utakuwa pia maalum kwa mastaa
kibao wakiongozwa na Diamond Platnumz.
Staa wa R&B kutoka Marekani, Shaffer Smith ‘Ne-Yo’.
“Historia inatarajiwa kuweka jijini Mwanza kwa
Ne-Yo kupiga shoo ya laivu kwa kutumia vyombo huku mastaa kibao kutoka
Bongo wakimsindikiza ambao ni Mo Music, Mr Blue, Fid Q, Stamina, Nay wa
Mitego na wengineo,” alisema Sebastian. Shoo hiyo imedhaminiwa na
Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom pamoja na Bahati Nasibu ya Shinda
Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment