April 06, 2016

                  

OFISI ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) imefafanua kuhusu mshahara wa Rais John Magufuli ikisema kuwa mishahara ya watumishi wa umma na viongozi wa umma hupangwa katika bajeti, hivyo mshahara wa Rais ni ule ulioidhinishwa katika Bajeti ya mwaka 2015/16.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dk Laurian Ndumbaro, bajeti ya mishahara yote ya watumishi wa umma na viongozi wa umma hupangwa kila wakati pale bajeti inapoandaliwa na kuidhinishwa na kwamba Rais mpya hakutengenezewa mshahara mpya.

Wizara yetu ndiyo yenye dhamana ya mishahara ya watumishi wa umma na viongozi wa umma, na hii huandaliwa kila mwanzo wa mwaka kabla ya kuanza kwa mwaka mpya wa fedha. Kwa hiyo mwaka 2015/16 fedha zake ziliidhinishwa Juni mwaka jana na kuanza kutumika Julai,” alisema Dk Ndumbaro.

“Kwa hiyo, bajeti hiyo iliidhinishwa kwa viongozi wote, Rais, Makamu wa Rais, wabunge na watumishi wote wa umma. Hivyo, mshahara wa Rais, kwa mantiki hiyo, Rais Kikwete (Jakaya) ndio huo ambao unatumiwa na Rais John Magufuli. Kama mshahara, hakuna tofauti, hakuna mabadiliko, kiwango ni kile kile. Rais mpya hakutengenezewa mshahara mpya,” alifafanua Katibu Mkuu huyo wa Utumishi na Utawala Bora.

Kumekuwapo na taarifa mbalimbali katika vyombo vya habari  kuhusu mshahara wa Rais na hivi karibuni, baadhi ya vyombo hivyo vilidai kuwa Rais mstaafu Kikwete alikuwa analipwa Sh milioni 34. 

Aidha, Rais Magufuli alikaririwa hivi karibuni akiwa nyumbani kwake Chato mkoani Kagera akisema kuwa analipwa mshahara wa Sh milioni 9.5 na akasema yupo tayari kuonyesha nyaraka zote.

Related Posts:

  • PAPA AWASILI UFILIPINO Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani,Mtakatifu Francis, amewasili nchini Ufilipino, nchi yenye Wakatoliki wengi zaidi barani Asia, huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa. Maelfu ya Wafilipino wamejipanga katika misur… Read More
  • NEW VIDEO: KIBOKO YANGU- MWANA FA ft ALLY KIBA Hii ni video mpya ya mkali Hamisi Corleone Mwinjuma aka Mwana FA ya Kiboko yangu ni moja kati ya ambazo zimekuwa zikisubiriwa kwa hamu na watu wengi. Video imetayarishwa na Director Kelvin Bosco wa … Read More
  • WATANZANIA WENGI WAFUNGWA HONG KONG Kasisi mmoja raia wa Australia amefichua na kuthibitisha kuwa kuna idadi kubwa ya wafungwa wenye asili ya Afrika katika magereza ya Hong Kong, wengi wao wakiwa ni kutoka Tanzania. Kasisi huyo John Wortherspoon ambaye … Read More
  • ABIRIA 60 WANUSURIKA KUZAMA ZIWA TANGANYIKA Ziwa Tanganyika. Abiria 60 kutoka Burundi na Jamhuri  ya Kidemokrasi  Ya Congo – DRC walionusurika katika ajali ya kuzama kwa boti katika ziwa Tanganyika wamewashukuru watanzania kwa kuwaokoa na ku… Read More
  • RONALDO DE LIMA KUREJEA DIMBANI Ronaldo de Lima anavyoonekana sasa. Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya brazil Ronaldo Luís Nazário de Lima anatarajia kurejea tena dimbani. De lima ameahidi kupunguza… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE