Kufanya kazi Ulaya ni raha sana kwa maana ya
kupiga hatua, lakini nako kuna ugumu wake kimaslahi kama utalifikiria suala la
kodi.
Najua unatamani kujua maisha ya wanasoka
wa Ubelgiji hususani katika kipindi hiki anachocheza soka
mtanzania Mbwana Samatta nchini humo,
Kwa mujibu wa mtandao
wa www.xpats.com hadi kufikia April 10 2015 mishahara ya
wachezaji wengi wa Ligi Kuu Ubelgiji ilikuwa inatajwa kuwa ya
wastani wa euro 253,586 kwa mwaka ambazo ni zaidi ya milioni 600 za
kitanzania kabla ya kukatwa kodi pamoja na bima.
Mshambuliaji mpya wa KRC Genk, Mbwana Samatta
atakuwa akilipwa mshahara wa euro 35,600 (zaidi ya Sh milioni 85) kwa mwezi.
Lakini makato ya kodi, kupitia kwa Mamlaka ya
Kodi ya Ubelgiji, yanamfanya Samatta kuondoka na kiasi kidogo tu cha kodi.
Taarifa za uhakika kutoka Ubelgiji zinasema,
Samatta atakuwa akikatwa asilimia 48 kama utajumlisha ‘TRA ya huko’ na makato
ya mshahara ya serikali ya mshahara wake. makato ambayo wanakumbana nayo wageni
wengi wanaofanya kazi nchini humo.
Pamoja na kulipwa zaidi ya Sh milioni 85,
maana yake Samatta atakuwa akipokea euri 18,200 (zaidi ya Sh 38,584).
kabla ya kutua KRC Genk, alikuwa akipokea
kitita cha dola 15,000 (zaidi ya Sh milioni 32) kutoka kwa TP Mazembe ambayo
aliitumia vizuri kujitangaza.
Maana yake kwa mshahara atakaokuwa akichukua
Samatta inaonekana hakuna tofauti kubwa sana na ule aliokuwa akichukua TP
Mazembe.
Lakini inawezekana alichoangalia zaidi ni
suala la hatua kwa ajili ya kupata mafanikio zaidi hapo baadaye kimshahara pia
kiuchezaji kwa ajili ya kutimiza ndoto zake.
Kwa mwezi huwa inatajwa
kufikia wastani wa euro 20000 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kitanzania.
Klabu ya Anderlecht iliyopo nafasi ya tatu katika Ligi, ndio inatajwa
kuwa klabu inayolipa mishahara mikubwa zaidi, kwa
mwaka Anderlecht inalipa hadi euro 600000 ambazo ni zaidi
ya bilioni 1.4 za kitanzania kwa mchezaji mmoja.
Klabu ya KRC
Genk anayocheza nahodha wa Taifa Stars Mbwana
Samatta inatajwa kuwa miongoni mwa vilabu tajiri ndani ya Ligi
Kuu Ubelgiji, ila kwa mujibu wa www.xpats.com, wachezaji wengi
wao Ubelgiji hulipwa kati ya euro 25000 hadi 50000 kwa mwezi.
KWa sasa, Samatta
ni mwanamichezo anayeshika nafasi ya pili kwa kulipwa mshahara mkubwa nyuma ya
Hasheem Thabeet ambaye alikuwa akichukua mshahara hadi dola 200,000 kwa mwezi
wakati akikipiga ndani ya NBA na sasa hata kama amepunguziwa kwa kuwa yuko ligi
ya chini, haiwezi kuwa chini ya dola 100,000 kwa mwezi.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment