Utaratibu
mpya bungeni ni wa timu maalum iliyopewa kazi maalum ya kurekodi matukio
ya Bunge yote yanayofaa kufikishiwa Wananchi na hayo matukio ndio
wanapewa waandishi wa habari ila hakuna tena utaratibu kama wa zamani
kwamba kila mwandishi anaweza kurekodi kwa Camera yake chochote
anachoona ni habari.
April 24 2016 Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania ‘JUHWATA’ limetoa tamko la mwenendo wa shughuli za bunge ambapo limeiomba
Serikali kama wameamua kuzuia bunge kutoonyeshwa pia waache kuonyesha
maswala yao ya Kiserikali kuweka usawa na kutoonyesha bunge na badala
yake muda huo wananchi wakafanye kazi za kujiingizia kipato badala ya
kuangalia vipindi vya live, mbele ya waandishi wa habari kupitia katibu
wa Jukwaa hilo, Mtela Mwampamba wameyazungumza haya……….
>>>‘tunaposema
kwamba Bunge lisionyeshwe live kwa sababu wananchi wanatakiwa wawe
kazini na serikali pia masuala yao ya kiserikali kama ufunguzi wa
daraja, ufunguzi wa Mwenge yasionyeshwe nayo live tusubiri yarekodiwe
ili wananchi waendelee kufanya kazi, kama wanaonyesha live labda iwe
sikukuu ya kitaifa’:-Mtela Mwampamba
Aidha
Jukwaa hilo limezungumzia tabia ya baadhi ya wabunge kususia mijadala,
vikao na shughuli nyingine za bunge kwa kuwa wamekuwa wakivunja katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara 63 (2) inayozungumzia uwezo wa
bunge na majukumu ya bunge wamesema……
>>>’tabia
hii ya kuendelea kususa inatunyima fursa sisi wananchi wa kawaida
kuweza kujua mawazo mbadala, tumekuwa tunapata mawazo ya upande mmoja
kwa sababu upande wa pili umekuwa na tabia ya kususa’ :-Mtela Mwampamba
Source:Millardayo.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment