Msanii mkongwe wa filamu, Brandina Chagula ‘Johari’ amesema nje ya
filamu anafanya biashara ya mapishi ya vyakula mbalimbali lakini ni kwa
oda maalum.
Muigizaji huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha
filamu ya ‘RJ Company’, akiwa Vicent Kigosi, amekiambia kipindi cha
Uhondo cha EFM kuwa, nje ya filamu yeye ni mjasiriamali wa biashara ya
chakula.
“Mimi kama mimi ni mjasiriamali, kwa sasa nafanya biashara ndogo
ndogo za maswala ya chakula yaani kupika. Kwa hiyo kama mtu akiwa na
ofisi yake alafu anataka huduma yangu ya chakula, naandaa alafu
nampelekea,” alisema Johari.
Johari amesema kazi hiyo amekuwa akiifanya kwa muda mrefu na
inampatia kipato kizuri kwa kuwa ni miongoni mwa kazi ambazo anazipenda
pia.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment