Mhe.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura (kushoto) akiongea na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Miss
Tanzania 2016/17 wakati wa kikao baina yao kilichofanyika mwishoni mwa
wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC)
mjini Dodoma. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Hashim Lundenga.
Picha na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Na Mwandishi Maalum – Dodoma
Wajumbe
wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 wameiomba Serikali iwasaidie kupata
wadhamini wa mashindano hayo kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa
kumi mwaka huu.
Ombi
hilo limetolewa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa kamati hiyo Hashim
Lundenga wakati akiongea na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokutana nao mjini Dodoma.
Lundenga
alisema changamoto kubwa inayowakabili hivi sasa ni kupata ufadhili wa
mashindano hayo ambayo yanafaida kwa mabinti wanaoshiriki hii ikiwa ni
pamoja na kujengewa uwezo wa kuwa viongozi wazuri wa baadaye.
“Mwezi
wa tisa warembo wanatarajiwa kuingia kambini watakaa huko kwa muda wa
mwezi mmoja ambako watapewa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja
kufundishwa jinsi ya kujitambua na kujiendeleza kielimu”, alisema
Lundenga.
Kwa
upande wake Mhe. Wambura aliwapongeza wajumbe wa kamati hiyo kwa
kuandaa mashindano hayo na kuwaahidi kushirikiana nao ili kuhakikisha
mashindano yanafanyika kama ilivyotarajiwa.
Mhe.
Wambura alisema, “Nawapongeza washiriki wa mashindano haya
walioiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Dunia kwani wameweza
kushika nafasi nzuri katika mashindano ya makundi mbalimbali pia
hawajawaangusha waandaaji wa mashindano kwa kuwa wanaendelea kuisaidia
jamii inayowazunguka.
Naye
Miss Tanzania, Lilian Kamazima alimshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa
kukubali kukutana nao na kusema kuwa mashindano hayo yanaumuhimu mkubwa
lisha ya washiriki kupewa zawadi mbalimbali lakini pia wakiwa katika
maandalizi ya mashindano wanafundishwa jinsi ya kuwa wanawake wa kuigwa
katika jamii, kuishi na kuisaidia jamii inayowazunguka.
Mashindano
ya Miss Tanzania Taifa yanatarajiwa kufanyika mwezi wa kumi, hivi sasa
mashindano ya vitongoji (Vituo) yanaendelea katika maeneo mbalimbali
nchini baada ya hapo yatafuatiwa na mashindano ya Kanda.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment