Leo maelfu ya wakazi wa Kanda ya Ziwa na Watanzania kwa ujumla
wanahuzuni kubwa kuwakumbuka watu zaidi ya 1,000 waliofariki katika
ajali ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba katika ziwa Victoria iliyotokea
miaka 20 iliyopita.
Tarehe 21 Mei 1996 mji wa Mwanza uligubikwa na simanzi ya kutisha,
uwanja uliozoeleka kwa shughuli za michezo wa Nyamagana ukageuzwa kwa
muda kuwa uwanja wa kupokelea miili ya watu waliopoteza maisha katika
ajali hiyo.
Tarehe hii meli ya MV Bukoba iliyokuwa ikitoa huduma katika
ziwa Victoria alizama kufuatia idadi kubwa ya watu waliokua wamepanda
katika meli hiyo.
Meli kubwa ya MV Bukoba iliyoundwa mwaka 1979 na ilikuwa na uwezo wa
kubeba mizigo tani 850 na abiria 430. Inaelezwa kuwa wakati meli hiyo
inazama ilikuwa na watu zaidi ya 1,000 ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya
uwezo wake wa kubeba abiria na ilizama umbali wa mita zipatazo 25 kutoka
ufukweni mwa maji na zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha.Wananchi hao waliofariki walizikwa katika makaburi ya Igoma Mkoa wa
Mwanza ambapo kila mwaka maadhimisho ya kumbukumbu ya kuwakumbuka ndugu zetu
waliopoteza maisha hufanyika.
Hii ni ajali kubwa kuwahi kutokea nchini kwa idadi kubwa ya watu
walipoteza maisha.
Achia mbali kupoteza maisha kwa watu hao wengi,
tunapokumbuka miaka 20 ya kuzama kwa MV Bukoba bado hakijapatikana
kivuko kingine imara cha kuweza kutoa huduma ya uhakika kama ilivyokuwa
MV Bukoba.

Makaburi ya wahanga wa ajali ya MV Bukoba.

TeamClouds ikiwakilisha kutoka Igoma kwenye makaburi ambako wapendwa wetu waliofariki kwenye ajali ya MvBukoba miaka 20 iliyopita wamepumzishwa hapa Shaffih EdgarKibwana Mkazuzu.tza daudiwakota

Mkuu wa Vipindi wa Clouds Fm shaffih Daudaakiweka shada la maua kwenyekjaburi

BrandManager wa XXL Hamis Mandi Bdozen akiweka shada katika kaburi

Mhe. Nape Nnauye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Napoe Nnauye akiwa na Mwanamitindo FlavianaMatata wakiangalia maonyesho ya vitendo vya usalama majini.
Wakazi wa Kanda ya Ziwa wamekua wakilia na Serikali kuweza kuwapatia
meli nyingine itakayotoa huduma kwani zilizopo sasa zinatoa huduma kwa
kusuasua sana na kufanya shughuli za uzalishaji kukwama wakati mwingine.
Ni imani yetu kuwa Watanzania tumejifunza kutokana na makosa
yaliyotokea katika kivuko cha MV Bukoba ili kuepusha madhara mengine
kama hayo. Kuzingatia sheria, taratibu na kanuni kutatusaidia kupukana
na madhara yasiyo yalazima.
Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment