May 21, 2016

Mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo, utaagwa siku ya Jumanne nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirisha kuelekea Same Mkoa Kilimanjaro kwa ajili maziko.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameeleza mazingira ya kifo cha Kabwe na kusema kuwa aliugua kwa muda mrefu tangu mwaka jana akenda India kwa matibabu na liporejea alikuwa mzima lakini siku za karibuni alilazwa katika hospitali ya Mama Ngoma Mwenge hadi umauti ulipomkuta.
Kabla ya hajashika wadhifa wa kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam marehemu Wilson Kabwe ameshawahi kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza na baada ya tuhuma kadhaa aliahamishwa na kuwa Mkurugenzi wa Jiji la  Dar es Salaam.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE