May 31, 2016

12224676_1683413261895812_1910400538_n
Mtayarishaji mkongwe wa muziki hapa Bongo, Master Jay amewajia juu wasanii wa Hip Hop bongo kwa kushindwa kutumia fursa zilizopo.
Miaka ya hivi karibuni muziki wa Hip Hop nchini umeonekana haulipi huku baadhi ya wasanii wa muziki huo wakigeukia kwenye muziki wa kuimba wakati kwenye list ya wasanii wanaoongoza kwa mkwanja duniani ni wasanii wa Hip Hop.
Akiongea na gazeti la Mtanzania, Master Jay alisema wasanii wa Hip Hop Bongo wanashindwa kutumia fursa zilizopo.
“Wana hip hop wa Kimarekani wengi wametumia muziki huo kutengeneza jina na jina lao ndilo lililotengeneza mafanikio yao tofauti na wana hip hop wa hapa Bongo, wanasubiri muziki uwalipe badala ya kuangalia na fursa nyingine kama wanavyofanya Wamarekani,” alisema.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE