
Kocha ajae Manchester
United, Jose Mourinho anategemewa kufanya mageuzi makubwa kwenye kikosi
cha timu hiyo kwa usajili wa wachezaji nyota utakaoigharimu timu hiyo
takriban pauni milioni 200 katika msimu huu wa usajili.
Mourinho anayeenda kuchukua mikoba ya Louis van Gaal aliyetimuliwa
Jumatatu, amewakeka katika orodha yake sentahafu John Stones wa Everton
na kiungo wa Chelsea Nemanja Matic.
Stone anatarajiwa kuigharimu Manchester United pauni milioni 45 wakati
Matic anatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25.
Mourinho pia anampigia hesabu beki wa Real Madrid Raphael Varane mwenye
thamani ya pauni milioni 45 pamoja na kiungo bab kubwa wa Sporting
Lisbon ya Ureno Joao Mario kwa pauni milioni 35.
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/05/mourinho-kufanya-kufuru-ya-usajili.html
Copyright © saluti5
Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/05/mourinho-kufanya-kufuru-ya-usajili.html
Copyright © saluti5
0 MAONI YAKO:
Post a Comment