May 24, 2016

samaki-galatone-559x520

Msanii Galatone ameweka wazi kuwa alishawahi kwenda kwa wa Waganga wengi wa kienyeji ili afanikiwe kwenye sanaa ya muziki anayoifanya., Galatone amesema ilifika kipindi alichoka katika harakati za kuuhangaikia muziki ndipo ikamlazimu kuingia katika nguvu za giza.“Nimefanya sana nimeenda kwa Waganga maana kuna kipindi nilichoka kabisa nkasema acha nikajaribu, nshavunja nazi, kuchinja kuku na kila kitu yani ili tu nitoboe kwenye game,” alisema.Galatone amekiri kuwa hakupata chochote na wala hakuona mabadiliko yoyote ndipo akaamua kuachana na mambo hayo na kumtegemeea Mungu tu.




Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE