May 11, 2016

 

Baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kunaswa na kamera akiidunisha Nigeria kuwa mafisadi wakuu kote duniani BBC imeamua kuangazia kwa umakini ikiwa matamshi hayo ni ya kweli.
Je Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ipi katika orodha ya mataifa fisadi kwa mujibu wa shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi duniani Transparency International ?
Ni vigumu kuelezea kwa kina ama hata kupiga msasa ufisadi katika mataifa kwani kila mwanauchumi anaelezea ufisadi akitumia mizani tofauti na mwenziye.
Kwa sababu hiyo tutatumia orodha ya mwaka wa 2015 ya shirikisho la kupambana dhidi ya ufisadi, Transparency International, ili kukupa taswira ya mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki na jinsi yanavyolinganishwa na mataifa mengine duniani katika mizani ya ubadhirifu na wizi wa mali ya uma.
Cha mno hata hivyo sharti tuweke bayana kuwa Nigeria sio taifa fisadi zaidi duniani.
Nigeria imeorodheshwa katika nafasi ya 136 Nigeria kati ya mataifa 167.
Kenya kwa mfano inasemekana kuwa na ufisadi mkubwa hata kuishinda Nigeria.
Katika kanda ya Afrika Mashariki , mali ya umma inafujwa sana na viongozi wa serikali hali ambayo inaiweka mataifa ya kanda katika nafasi za mwisho mwisho kuashiria viwango vya juu vya ufisadi.
Kati ya mataifa kumi Fisadi zaidi duniani Somalia inaongoza ikifwatwa na Sudan ,Sudan Kusini, Eritrea, Burundi, DRC, Uganda, Kenya Tanzania Ethiopia na kisha Rwanda katika usanjari huo.
Somalia inaongoza kwa Ufisadi duniani katika nafasi ya 167.
Viwango vya ufisadi vinanasibishwa na Korea Kaskazini.
Taifa hilo linaloongozwa na rais Paul Kagame linaorodheshwa katika nafasi ya 44 duniani.
Je unakumbuka rais Robert Mugabe aliyewadunisha wakenya kwa kuwa wezi ?
Kulingana na orodha hii iliyotayarishwa na shirika la TI Zimbabwe wanaorodheshwa katika nafasi ya 150 duniani kwa ufisadi.
Wanagawana nafasi hiyo na Burundi.
Orodha ya mataifa 10 fisadi zaidi kanda ya Afrika Mashariki na Duniani.
1. 167 Somalia / North Korea
2. 165 Sudan
3. 163 South Sudan/ Angola
4. 154 Eritrea/Yemen / Turkmenistan / Syria
5. 150 Burundi / Zimbabwe
6. 147 Democratic Republic of the Congo / Chad / Myanmar /
7. 139 Kenya / Uganda
8. 117 Tanzania
9. 103 Ethiopia
10. 44 Rwanda
Nchi iliyojitenga kabisa na ufisadi kanda ya Afrika Mashariki na kati ni Rwanda.

Related Posts:

  • Papa Benedict XVI aeleza sababu za yeye kujiuzulu Papa Mtakatifu Benedict XVI alipokuwa akihojiwa alisema kuwa aliona kujiuzulu kwa ke lilikuwa ni jambo la lazima kutokana na kuporomoka kwa afya yake na kushindwa kuendana na kasi ya kazi zake. Japo alitamani… Read More
  • Rais Magufuli atishia kubadili noti za fedha. Septemba Mosi 2016 Rais Magufuli amezungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa mlimani City jijini Dar es salaam. Katika kile kinachoonekana ni kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa… Read More
  • Afande Sele Mikononi Mwa Polis Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele amedai anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa madai anagawa pesa kwa watu ili kuwashawishi wajitokeze katika maandamano ya UKUTA ambayo yamepigwa ma… Read More
  • Kurasa za Magazetini leo hii September 01 Karibu  katika kurasa za magazetini leo hii ikiwa ni 01 September 2016 huku Tanzania ikiingia katika Historia ya Dunia ya kupatwa kwa jua . Magazeti ya leo yamebebwa na habari hizi kubwa … Read More
  • Video rasmi ya Raymond Natafuta kiki hii hapa    Ni miongoni mwa waimbaji wa bongo wanaopewa sifa nyingi za utunzi na uimbaji kwenye bongofleva, lebo inayomsimamia ni WCB ya Diamond Platnumz, ukishamaliza kuitazama hii video usiache kutoa comment yako … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE