May 31, 2016

dsm
 Wanafunzi wa chuo kikuu cha cha Dar es salaam (Udsm) mpaka sasa wamegoma wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha kwa ajili ya kujikimu.
Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshengema amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizokuwa zikitolewa na bodi juu ya lini fedha hizo zitatolewa.
Kwa kawaida pesa ya chakula huingiziwa kila baada ya siku 60 na mpaka sasa yapata wiki mbili pasipo kupatikana. Mgomo huo unakuja zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Rais Magufuli kuzulu chuo hicho kwa ajili ya uzinduzi wa jengo la Maktaba.
Source: Mwananchi



0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE