Akaunti ya Instagram ya Linah yenye followers milioni 1.3 imedukuliwa (hacked) Jumanne hii.
Tayari hacker huyo ameibadilisha jina akaunti yake na kuipa jina
‘same_hacker’ huku akifuta picha zake zote alizoziweka mwaka huu.
Post ya mwisho inayoonekana sasa ni video ya tamthilia ya Empire
aliyoiweka December 27, 2015. Haijulikani nini lengo la hacker huyo na
kama ni wa hapa hapa Tanzania.
Linah anakuwa msanii wa hivi karibuni ambaye akaunti yake ya
Instagram imedukuliwa. Miezi kadhaa iliyopita akaunti ya Shilole pia
ilidukuliwa japo alifanikiwa kuirejesha.
“Jamani daaaah ndo kama hivyo watu washafanya yao pole kwa uwezo wa Allah itarudi,” Shishi amempa pole Linah.
Zaidi ya kujitangaza, miaka ya hivi karibuni akaunti za mastaa
zimekuwa moja ya vyanzo vyao muhimu vya kipato na wale wenye followers
wengi wamekuwa wakipata deals zenye hela nyingi.
Ni wazi Linah atakuwa kwenye wakati mgumu kwa sasa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment