Kiongozi wa chama cha upinzani cha CUF, Seif Shariff Hamad.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha CUF kisiwani Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema
vyama vyenye nguvu vya upinzani vinahitajika pamoja na tume ya uchaguzi
ilio huru ili kushinda marais walioko madarakani.
Seif Shariff Hamad ameongeza kuwa waafrika lazima wahakikishe kuwa
jeshi pamoja na vikosi vingine vya usalama vinawekwa mbali na siasa kwa
kuwa mara nyingi vinatumika kusaidia chama tawala.
Zanzibar ni kisiwa ambacho ni sehemu ya Tanzania pamoja na visiwa
vingine viwili, vidogo kwenye Bahari Hindi karibu na ufukwe wa Tanzania.
Mwezi Machi mwaka huu, Zanzibar ilifanya uchaguzi wa marudio ya
uchaguzi wa Oktoba mwaka jana lakini chama cha CUF kilisusia kwa kuwa
kiliamini kuwa mgombea wake Hamad alikuwa ameshinda kwenye uchaguzi wa
awali.
Hamad sasa hivi yuko kwenye ziara hapa mjini Washington kukutana na viongozi wa Marekani kuhusu hali ya kisiasa ya Zanzibar.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment