June 15, 2016

 
 
 Taarifa zilizotufikia ni kwamba Basi la Abiria la kampuni ya TAHMEED linalofanya safari zake kati ya Tanga Na Dar es salaam limeteketea kwa.moto katika barabara ya chalinze segera

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa hakuna mtu aliyefariki wala kujeruhiwa kutokana na ajali hiyo lakini mizigo ya abiria ndiyo imeteketea ndani ya basi hilo.

Ajali imetokea wakati basi hilo limesimama baada ya abiria mmoja kuomba msaada akajisaidie na ndipo abiria waliokuwamo ndani ya gari alianza kusikia harufu ya moshi wa tairi linaloungua na ndipo wakatoka nje ya gari wote na muda mfupi gari lote likashika moto.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE