June 15, 2016



Sote tunajua kuwa Prof Lipumba ni msomi mahiri wa uchumi duniani, ana mchango mkubwa usiopingika na usio na shaka katika UJENZI WA DEMOKRASIA YA MFUMO WA VYAMA VINGI NCHINI. Amefanya kazi kubwa mno ya kuijenga CUF na kuonyesha kuwa yeye ni mfano mzuri wa kuigwa miongoni kwa wasomi wengi walioshindwa kujitoa muhanga katika kipindi cha mwanzo wa kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini 1995, aliachana na ajira na kuungana na makabwela kwa madhumuni ya kuwaunganisha watanzania kudai HAKI SAWA KWA WOTE.
BADO CUF INAMUHITAJI SANA PROF. LIPUMBA KUWA MSHAURI, NA MZEE WA CHAMA ILI KUFIKIA AZMA YA TAASISI YETU KUKAMATA KHATAMU ZA DOLA KWA MADHUMUNI YA KULETA MABADILIKO YA KWELI YA KIMFUMO NA KIUONGOZI ILI KUHARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA LETU NA WATU WAKE.
Prof. Lipumba anauwezo na nafasi kubwa ya kuendelea kukitumikia CHAMA na tumeliona hilo hakuna kiongozi yeyote aliyepingana na hilo mbali na kujiuzuru kwake aliendelea kufanya mikutano na waandishi wa Habari ofisi kuu ya CUF Buguruni na kujumuika katika hafla mbalimbali za CUF na kualikwa katika vikao vyà maamuzi ikiwemo BARAZA KUU LA UONGOZI TAIFA hali ya kuwa si Mwenyekiti wa Taifa wa CHAMA kutokana na kujiuzuru kwake.
Katibu Mkuu wetu Maalim Seif amekuwa karibu nae mara zote kwa kipindi chote hicho kwa kushauriana na kufarijiana hata pale Maalim Seif alipokuwa amelazwa Hindu Mandal na baadae kupumzika Serena Hotel.

Hakuna kitu kikubwa katika taasisi yeyote na MTU binafsi kama kujenga na kuwa na TASWIRA (POSITIVE IMAGE) inayokubalika katika jamii unayoitumikia au unayotaka kuitumikia. Jinsi utakavyo iweka Image yako ndivyo inavyoweza kukujenga au kukubomoa. Wakati mwingine Image unaweza kuifasiri kama Trust (Imani)
Siasa za nchi yetu zimebadilika Sana. Maamuzi ya CHAMA juu ya nani anaongoza Taasisi yanajadilika na jamii pana sana ya watanzania ambao ni wapiga kura zaidi ya milioni 6 wanaounga mkono siasa za mageuzi na au mabadiliko (vyama vya upinzani). Khususani kwa vyama vya CUF, CHADEMA NA NCCR. Suala la uenyekiti wa Taifa wa CUF kwa sasa kutokana na hiyo "dynamism and reflection of 2015 general election" ni la watanzania wote wapenda mabadiliko na si la wanaCUF pekee.
Wakati mwengine MTU mzima au wazee wetu wakiteleza katika jambo si lazima aje atuombe radhi sisi watoto zake.
Kuonyesha dhamira ya kutaka kuendelea na mapambano iñatosha. Na nimjuavyo Mimi Prof anauwezo wa kupambana na watawala wenye element za kifashisti na kidikteta kama ilivyokuwa kwa wakati ule wa utawala wa serikali ya awamu ya tatu ya Benjamin William Mkapa, nae kama trend anayotaka kuifuata huyu JPM, Mkapa alitaka kuzuia shughuli za siasa zisifanyike baada ya uchaguzi Mkuu 2000. Prof. Alisimama NGANGARI mpaka Haki ikapatikana PAMOJA na kutokea mauaji ya ndugu zetu January 26/27. Nikikumbuka na kutaja mazuri machache aliyoifanyika CUF NA WATANZANIA KWA UJUMLA.
Naomba kuhitimisha mchango na maoni yangu fikra katika ukuta huu kwa kusema ifuatavyo;
TUACHE MKUTANO MKUU WA TAIFA WA CUF UFANYIKE NA TUPATE SAFU MPYA YA UONGOZI WA CHAMA TAIFA TAYARI KUJIPANGA KUTUPELEKA MWAKA 2020 HUKU MAPAMBANO YA KUDAI NA KUHAKIKISHA HAKI YA WAZANZIBARI INAPATIKANWA KWA WAKATI.
TUNAMUHITAJI SANA PROF.LIPUMBA Kuendelea kukitumikia CHAMA chake cha CUF NA KUUNGANISHA NGUVU ZAKE NA UONGOZI MPYA WA CHAMA UTAKAOPATIKA MWEZI AUGUST akiwa ni MWANACHAMA HAI, NGANGARI, MSHAURI NA KIONGOZI MUELEKEZI KATIKA MASUALA MBALIMBALI YA KISIASA, KIUCHUMI, KIJAMII NA KIMKAKATI KWA MASLAHI YA CUF NA TAIFA LETU KWA UJUMLA.
Na ikizingatiwa kuwa utawala huu wa JPM una muelekeo na viashiria tosha vya kusudio la ukandamizaji wa Demokrasia nchini.
UMOJA NI NGUVU, NA UTENGANO NI UDHAIFU.
HAKI SAWA KWA WOTE.
Na, Mbarala Maharagande

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE