June 07, 2016



Ndugu zangu waandishi wa habari,
Katika siku za hivi karibuni, Jeshi la Polisi nchini, limepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa wakitaka kufanya mikutano na maandamano . hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia vyanzo vyake vya mbalimbali vya habari limebaini kuwa mikutano hiyo ina lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi (Civil disorder).

Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao.

Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.

Kwa hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia tarehe 07/06/2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.

Jeshi la Polisi linawataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi.

Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.

Aidha Jeshi la Polisi linawataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.

Asanteni sana kwa kunisikiliza .

Imetolewa na:-
Nsato M. Mssanzya – CP
Kamishina wa Polisi Operesheni na Mafunzo
Makao Makuu ya Polisi.

Related Posts:

  • New Audio| I do - Caleedy ft Braitz Anaitwa Caleedy, ni mwanamuziki chipukizi toka mkoani Morogoro, amekuletea wimbo wake unaoitwa I do. Caleedy katika wimbo huu amemshirikisha mkali wa wimbo wa Deka anayefahamika kwa jina la Braitz. wimbo umefanywa na Pro… Read More
  • Jose Mara na siri ya kufanana majina na mkeweMakala: MUSA MATEJA KILA mtu ana historia yake katika maisha! Joseph Michael ‘Jose Mara’ yeye kutokana na historia ya kimaisha aliyopitia, amesema mkewe Monica Michael Joseph ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu. KWA NINI NI Z… Read More
  • Karibu katika magazeti ya leo january 9 2016 Karibu ndugu mwana familia wa Ubalozini.blogspot.com upate kupitia japo vichwa vya habari vya magazeti yetu leo hii. Ukitaka habari kwa undani pitia katika meza za magazeti … Read More
  • Vipindi vya watu wazima mchana marufuku   Mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya imechapisha mwongozo mpya wa vipindi vya radio na televisheni. Mwongozo huo unanuia kudhibiti nyakati za kupeperusha matangazo na vipindi vinavyolenga watu wazima na pia kuepusha… Read More
  • Serikali imesitisha zoezi la bomoabomoa isipokuwa ...   Serikali imesitisha zoezi la bomoabomoa katika maeneo mbalimbali isipokuwa katika eneo la bonde la mto msimbazi ambalo linaanzia katika vilima vya pugu hadi daraja la salender jijini Dar es Salaam ambalo hata hivy… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE