Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Ndugu. Zitto Kabwe ameandika katika ukurasa wake wa Facebook na kusema fedha za Marekani ni Porojo
Fedha za Marekani? Ni porojo tu. Kila senti ambayo nchi inapata huingizwa kwenye kitabu hiki ambacho kila mbunge hupewa. Ni Revenue Book Vol 1. Katika Bajeti ya mwaka huu hakuna hata senti ya kutoka Marekani. Rais na Balozi wa Marekani wamedanganyana tu au Wamarekani wataweka fedha zao kupitia makampuni Yao ya Kimarekani. Bunge ndio lenye mamlaka ya juu kupitisha mapato na matumizi ya Serikali. Hizo hela za Marekani ambazo watu wanazishangilia ni HEWA. Ni POROJO
0 MAONI YAKO:
Post a Comment