June 05, 2016

Kocha wa Zimbabwe Kalisto Pasuwa, anatarajiwa kurithi nafasi ya Mganda Jackson Mayanja, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe kuwa katika mazungumzo ya mwisho ili kumalizana naye.
Hans Poppe amesema, anauhakika Pasua atatua msimbazi kutokana na kukubali ofa waliyompa ambayo hajaitaja kwa ajili ya kuifundisha timu yao msimu ujao.
“Nikocha mwenye uwezo mkubwa ndiyo maana taifa lake likamuamini na kumpa timu ya taifa, ujio wake tunaimani ataweza kuvunja nguvu za wachezaji wa Yanga Donald Ngoma na Thabani Kamusoko,”amesema Hans Poppr.
Mbali na kocha huyo Hans Poppe amesema wanatarajia kusajili mshambuliaji mmoja hatari kutoka nchini humo ambaye pia anaichezea timu ya taifa.
Hans Poppe alisema Simba inaendelea kujiimarisha kwa kuangalia ambacho wanahitaji baada ya Kocha Jackson Mayanja kukabidhi ripoti.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE