June 13, 2016

Linah
Msanii mahiri wa muziki, Linah Sanga amesema hatafanya tena makosa ya kusaini mkataba na label yoyote kama alivyofanya makosa katika kipindi cha nyuma.

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kutamba na wimbo ‘Ole Themba’, mara ya mwisho alikuwa chini ya label ya muziki ya ‘Pan Musiq’ ambapo alifanikiwa kufanya project kadhaa ikiwemo ya ‘No Stress’.
Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Linah amesema amechoka kuhamahama katika label.
“Kuna label nyingi sana zinataka kufanya kazi na mimi,” alisema Linah. “Lakini mimi bado siko tayari kwa sababu nimeshapita katika label kama tatu au nne na nimeshaona ugumu uliopo. Sitaki tena kufanya makosa kwa sababu sipendi ile hali ya kuhamahama , kwa hiyo nahitaji label ambayo nitakubaliana nayo kwenye kila kitu,”
Muimbaji huyo ambaye hivi karibuni ameachia video ya wimbo ‘Imani’, amesema kwa sasa anakabiliwa na ukata wa pesa hali ambayo inamfanya ashindwe kuachia kazi zake kwa wakati.





0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE