June 12 2016 chama cha ACT-Wazalendo kilikutana na waandishi wa habari kutoa taarifa kuhusu Kongamano lao la Bajeti walilokuwa wameliandaa kuzuiwa na polisi.
Taarifa hiyo waliyoitoa ilisema kwamba katika kongamano hilo walilenga kumpa fursa ya pekee kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe kusema yale ambayo angeyasema bungeni baada yeye na wabunge wenzake sita wa upinzani kusimamishwa kuhudhuria vikao vya bajeti bungeni.
Zimekuwepo taarifa ya kwamba Kiongozi wa chama hicho Zitto Kabwe amekuwa akitafutwa na polisi bila mafanikio, hapa amejitokeza mbele ya waandisha wa habari na kuzungumza haya…..>>>’hii ya jumamosi ilikuwa ni kama kunivizia na watu wa usalama wa chama wakawa wamechukua hatua za kuzuia’
>>>tukawa tumehisi kwamba nia yao ya kutaka kunikamata ni kuhakikisha kwamba sitakuwepo kwenye kongamano tukachukua hatua ili wasiweze kunikamata ili tuweze kuendelea na kongamano nadhani sababu ya hasira ya kutonipata au lengo lao la kuzuia mikutano ambao wameizuia wakazuia kongamano letu’
Kutazama Full video ya Zitto Kabwe, bonyeza play hapa chini
0 MAONI YAKO:
Post a Comment