Mkali wa wimbo ‘Moyo Mashine’, Ben Pol amefunguka na kuzungumzia
hatua ya Diamond Platnumz kumsani msanii kubwa kama Rich Mavoko katika
label yake WCB.
Akiongea na Bongo5 hivi karibuni, Ben Pol amesema hatua ya Diamond
kuamua kumsaini Rich Mavoko katika label ya WCB, itafungua njia kwa
wasanii wengine kuwa na moyo wa kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.
“Ni vizuri sisi kwa sisi tukaaminiana na kufanya kolabo kwenye kazi,”
alisema Ben Pol. “Diamond ni mpiganaji na Mavoko ni mtu ambaye ana
kipaji na mjanja mjanja, kwa hiyo muungano wao unaweza kuleta mapinduzi
makubwa katika muziki,”
Pia muimbaji huyo amewataka wale wasanii wenye uwezo wa kuwasaidia
wenzao wasisite, kwani hiyo ndiyo njia sahihi ya kuupeleka muziki wa
Tanzania mbele zaidi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment