June 29, 2016

Madrasa yachomwa moto Uswidi

Madrasa moja katika eneo la Vaxjo kusini mwa Uswidi ambapo watoto hupewa  mafunzo ya kiislam imeripotiwa kuchomwa katika usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.

Taarifa hiyo ilitolewa na kituo cha runinga cha SVT na Polisi kuripoti kuwa tukio hilo ni la uhalifu.

Kikosi cha zima moto kilichokuwa na watu 25 kilifaulu kuzima moto huo kwa muda wa masaa matatu.

Ifahamike ya kwamba watoto wapatao 200 kutoka katika nchi 6 wanapewa mafunzo katika madrasa hayo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE