Taarifa
zafahamisha kwamba shirika la kifaransa la usalama wa anga (BEA)
limeanzisha utafutaji wa mabaki ya ndege ya EgyptAir iliyoanguka katika
bahari ya Mediterania mwezi uliopita.
Shughuli hiyo ya utafutaji itafanyika kwa usaidizi wa roboti inayotumika katika maji ya kina .
Misri imeajiri kampuni ya kibinafsi ya Deep Ocean inayohusika na kazi za kutafuta vitu katika bahari.
Hata hivyo eneo ambalo ndege hiyo ilipoangukia linakadiriwa kuwa na urefu wa mita 3,000.
Ndege hiyo ilipotea katika skrini za rada ilipoanguka kati ya kisiwa cha Ugiriki na pwani ya Misri.
Aidha chanzo cha ajali ya ndege hiyo bado hakijabainika huku kukiwa na tetesi za uwezekano na shambulizi la kigaidi na pia hitilafu za kimitambo.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment