Washtakiwa
sita wanaokabiliwa na makosa tofauti yakiwemo ya kubaka, kulawiti na
kusambaza picha chafu na za ngono wameendelea kusota rumande kwa kukosa
dhamana, baada ya mvutano mkali wa mawakili wa upande wa mashtaka na
upande wa washtakiwa kuibuka mahakamani hapo, na hakimu anayesikilisha
shauri la dhamana kuahirisha shauri hadi Juni 15 mwaka huu kutoa uamuzi
juu ya dhamana.
Miongoni
mwa washtakiwa hao, wawili,Iddi Adam Mabena (21) mkazi wa Njombe na
Zuberi Thabit (30) mkazi wa Mbarali Mbeya wanaokabiliwa na shtaka la
kumbaka na kumlawiti binti mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Wami
Dakawa,wilayani Mvomero wanalodaiwa kutenda Aprili 27 mwaka huu majira
ya usiku katika nyumba ya kulala wageni ya titii iliyopo wami dakawa
wilayani mvomero,shauri lao linalosikilizwa faragha limeahirishwa tena
mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya mkoa wa Morogoro Mary
Moyo.
Upande
wa mashtaka katika shauri hilo linalosikilizwa faragha kwa mujibu wa
sheria, umewakilishwa na waendesha mashtaka Gloria Rwakibalila,Edgar
Bantulaki,Calistus Kapinga na Mohamed Mkali na limepangwa kufikishwa
tena mahakamani hapo Juni 15 mwaka huu kwaajili ya kuanza usikilizwaji
wa awali baada ya upelelezi kukamilika.
Uamuzi
wa dhamana itolewe ama isitolewe umeshindwa kufikia muafaka baada ya
mvutano wa kisheria wa mawakili wa utetezi na wa Jamhuri, katika shtaka
la kusambaza picha chafu na za ngono kwa njia ya mtandao kinyume na
sheria ya makosa ya mtandao no 14 ya mwaka 2015, linalosikizwa mbele ya
hakimu Ivan Msaki,wa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro,dhidi ya
washtakiwa sita,iddi Mabena na Zuberi Thabit,wanaotetewa na wakili
Mohamed mkali,na Rajab Salehe,Ramadhani Ally Makunja, Muhsin Ngai na
John Peter Thabiti maarufu kama paroko, wakazi wa wami dakawa wilayani
Mvomero wanaotetewa na wakili Ignas Punge.
Upande
wa mashtaka umeendelea kutetea uamuzi wake wa kuwasilisha kiapo cha
kupinga dhamana kwa vile shauri hilo limevuta hisia ya watu, usalama wao
utakuwa mashakani wawapo uraiani hasa ikizingatiwa wanadaiwa
kudhalilisha utu wa mwanamke na kutoharibu upelelezi kwa vile bado
haujakamilika,na kwamba taarifa za kiintelijensia zimebainisha
wakiachiwa huru wanaweza wakadhuriwa na jamii.
Hata
hivyo upande wa utetezi uliowasilisha hati kupinga kiapo hicho umedai
dhamana ni haki ya mshtakiwa,hakuna raia aliyewasilisha kiapo kuhusu
hasira kali alizonazo dhidi ya washtakiwa isipokuwa labda ni hisia za
mkuu wa upelelezi wa mkoa.
Hakimu
Ivan Msaki ameahirisha shauri hilo hadi Juni 15 mwaka huu ambapo uamuzi
wa washtakiwa kupewa dhamana au kunyimwa dhamana utajulikana.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment