Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanza kuwakupa pensheni kwa wazee wote wenye umri wa kuanzia miaka sabini ili kukabiliana na hali mbaya ya kiuchumi inayowakabili wazee waishio visiwani humo.
Leo wazee wamepanga foleni na kupewa fedha hizo ambapo wamesema kuwa zitawasaidia kujikimu kwani wamekuwa wakipatashida kwa wakati mwingine kukosa msaada na wao hawawezi kufanya kazi.Katika utaratibu huu unaonekana kuwasaidia wazee inaelezwa kuwa wazee elfu ishirini watanufaikia na mpango huo ambapo kila mmoja atapatiwa kiasi cha dola 9 ambozo ni sawa na shilingi elfu 19 kila mwezi huku kiwango cha pensheni kikitarajiwa kupanda kulingana na hali ya uchumi itakavyokuwa.
Aidha, utaratibu huu utawasaida wazee ambao wengi wamekuwa wakikalbiliwa na hali ngumu ya maisha. Licha ya wazee kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi, wao ndio wamekuwa walezi wa kundi kubwa la wajukuu ambao wengi wao ni watoto yatima, sambamba na kuwa na jukumu la kuhudumia watoto na wajukuu wao walioathirika kwa ugonjwa hatari wa ukimwi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment