July 31, 2016

 
TAMASHA la muziki wa bendi za Tanzania (Tanzania Band Festival) lilifanyika Jumamosi usiku katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kupokewa kwa msisimko wa aina yake. Bendi kama Msondo Ngoma, Sikinde, B Band, Akudo, FM Academia, Skylight, Twanga Pepeta, Yamoto na nyingine nyingi, zikapata wasaa wa kuonyesha ufundi wao jukwaani. Haikuwa mashindano, bali lilikuwa ni tamasha lililodhamiria kuleta mshikamano na mingoni mwa bendi zetu, hususan zile za muziki wa dansi. Kama mapungufu kadhaa yaliyojitokeza yatafanyiwa kazi vizuri, basi tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika kila mwaka, litakuwa ni jukwaa muhimu ya kuukwamua muziki wa dansi. Waandaaji wa onyesho hilo, Q Plus General Enterprises wanapaswa kupongezwa na kuungwa mkono badala ya kukatishwa tamaa kutokana na ukweli kuwa kuzikutanisha bendi nyingi kiasi kile maana yake ni kwamba unazungumzia matumizi ya uwekezaji mkubwa wa pesa. Mpangilio wa show ulikuwa kama ifuatavyo: TOT Band walifuangua pazia kisha wakafuata Akudo Impact, Sikinde, QS Internationa Band, King Kiki, Family Team, Msondo, Yamoto, B Band, Top Band, Skylight Band, Mapacha Watatu, Twanga Pepeta kisha pazia likafungwa na FM Academia. Onyesho lilianza rasmi majira ya saa 12 jioni na kuendelea hadi saa 10 za alfajiri. Mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Paul Makonda ambaye alichangia zawadi ya shilingi milioni moja. Pata picha za onyesho hilo la Tanzania Band Festival. 
  
B Band

 
Shaban Dede kushoto akiwa na Zomboko
 

Family Team

 
Mc wa show bwana Hamis Dacota toka Clouds Media

Picha zaidi  Bofya hapa
MC wa onyesho alikuwa ni Khamis Dacoto wa Clouds FM/Clouds TV

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/07/picha-38-za-tanzania-band-festival.html
Copyright © saluti5
PICHA 38 ZA TANZANIA BAND FESTIVAL NDANI YA LEADERS CLUB A+ A- Print Email TAMASHA la muziki wa bendi za Tanzania (Tanzania Band Festival) lilifanyika Jumamosi usiku katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kupokewa kwa msisimko wa aina yake. Bendi kama Msondo Ngoma, Sikinde, B Band, Akudo, FM Academia, Skylight, Twanga Pepeta, Yamoto na nyingine nyingi, zikapata wasaa wa kuonyesha ufundi wao jukwaani. Haikuwa mashindano, bali lilikuwa ni tamasha lililodhamiria kuleta mshikamano na mingoni mwa bendi zetu, hususan zile za muziki wa dansi. Kama mapungufu kadhaa yaliyojitokeza yatafanyiwa kazi vizuri, basi tamasha hilo ambalo limepangwa kufanyika kila mwaka, litakuwa ni jukwaa muhimu ya kuukwamua muziki wa dansi. Waandaaji wa onyesho hilo, Q Plus General Enterprises wanapaswa kupongezwa na kuungwa mkono badala ya kukatishwa tamaa kutokana na ukweli kuwa kuzikutanisha bendi nyingi kiasi kile maana yake ni kwamba unazungumzia matumizi ya uwekezaji mkubwa wa pesa. Mpangilio wa show ulikuwa kama ifuatavyo: TOT Band walifuangua pazia kisha wakafuata Akudo Impact, Sikinde, QS Internationa Band, King Kiki, Family Team, Msondo, Yamoto, B Band, Top Band, Skylight Band, Mapacha Watatu, Twanga Pepeta kisha pazia likafungwa na FM Academia. Onyesho lilianza rasmi majira ya saa 12 jioni na kuendelea hadi saa 10 za alfajiri. Mgeni rasmi alikuwa ni mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Paul Makonda ambaye alichangia zawadi ya shilingi milioni moja. Pata picha 38 za onyesho hilo la Tanzania Band Festival.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/07/picha-38-za-tanzania-band-festival.html
Copyright © saluti5

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE