July 03, 2016

Polisi wavamia ofisi kuu za chama cha upinzani Zambia
Maafisa wa polisi nchini Zambia wameripotiwa kuvamia ofisi kuu za chama cha upinzani katika mji mkuu wa Lusaka.
Maafisa hao wanaarifiwa kuharibu stakabadhi za kampeni za uchaguzi zilizokuwa zimeandaliwa na upinzani kwa kudaiwa kulenga kuchochea wananchi.
Viongozi wa upinzani walitoa maelezo na kuarifu kwamba polisi waliojihami kwa silaha walitekeleza uvamizi kwenye ofisi kuu za chama cha UPND.
Katibu mkuu wa UPND alitambulisha tukio hilo kuwa kama unyanyasaji wa serikali dhidi ya upinzani kwa kutaka kuvuruga mipango yao ya kampeni kufuatia uchaguzi wa Agosti 11.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE