July 05, 2016

image


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka  aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act)  Sura 1, leo tarehe 5 Julai, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB Prof. William Lyakurwa.
Kufuatia hatua hiyo, kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (2) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act) Sura 257, Mhe. Rais amemteua Prof. Palamagamba J. A. M. Kabudi kushika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB kwa kipindi cha miaka mitatu.
Kufuatia mabadiliko hayo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango  kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act)  Sura 1,  ametengua uteuzi wa Wajumbe Bodi ya Benki ya Maendeleo ya TIB. Aidha,  kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 9 (1) cha ya Sheria ya mashirika ya umma (Public Corporations Act, Sura 257) Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango ameteua wajumbe wapya wa Bodi wafuatao kwa kipindi cha miaka mitatu:
  1. Gen (Rtd) Mabula Mashauri
  2. Razack B. Lokina
  3. Rose Aiko
  4. Joseph Bwechweshaija
  5. Said Seif Mzee
  6. Arnold M. Kihaule
  7. Maduka Paul Kessy
  8. Charles Singili
Uteuzi  wa Mwenyekiti na Wajumbe wapya wa Bodi unaanza tarehe leo 5 Julai, 2016.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
05 Julai, 2016.

Related Posts:

  • Serikali kuwarudisha watanzania toka A.Kusini-Membe    Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe amesema mpaka sasa hakuna mtanzania aliyefariki kutokana na vurugu wanazofanyiwa raia wa kigeni nchini Afrika Kusini. Akizungumza na wana … Read More
  • Rwanda kuandaa CECAFA   Kocha mmoja wa Rwanda  Rwanda imeteuliwa kuwa mwenye wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFGA Challenge Cup, Novemba mwaka huu. Katibu mkuu wa CECAFA Nicholas… Read More
  • Jaguar awatibua mashabiki Marekani   Msanii wa kenya Jaguar Mwanamuziki wa Kenya Charles Njagua kanyi anayejulikana kama 'Jaguar' alitarajiwa kuwatumbuiza raia wa Atlanta nchini Marekani siku ya ijumaa lakini hakuonekana hadi asubuhi ya siku ya ju… Read More
  • Hii ndiyo list ya walioingia tano bora tuzo za watu 2015 1-Video ya muziki inayopendwa  TZW13 Akadumba - Nay  Kipi Sijasikia – Prof J  Nani kama Mama – Bella  Wahalade - Barnaba  XO - Joh Makini  … Read More
  • Msanii jela kwa kukejeli bendera ya Taifa   Msanii mmoja wa kucheza dansi , raia wa Armenia nchini Misri, amehukumiwa kifungo cha miezi sita gerezani, kwa madai ya kutusi bendera ya taifa hilo. Msanii huyo anayefahamika kama Safinas, alihukumiwa kwa kosa l… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE