Vituo vinavyotoa huduma ya tiba mbadala, Foreplan Clinic cha Dr Juma Mwaka na kile cha Fadhaget Sanitarium Clinic vimefungiwa.
Uamuzi huo umechukuliwa na baraza la tiba za asili na tiba mbadala
kwa madai kuwa vituo hivyo vimekiuka masharti ya vibali walivyokuwa
wamepewa.
Limesema wamiliki wamekuwa wakitangaza kuwa wanatoa tiba za kisasa badala ya zile za asilia.
Akiongea na waandishi wa habari Jumanne hii jijini Dar, mwenyekiti wa
baraza hilo, Dk Edmund Kayombo alitangaza kufuta usajili wa vituo
hivyo. Hiyo inamaanisha kuwa vituo hivyo havitakiwi kutoa huduma hiyo
tena.
Kituo kingine kilichokutana na rungu hilo ni Mandai Herbal Clinic.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment