Mkali wa wimbo ‘Mboga Saba’ Mr Blue amedai kuwa mtindo wa
kuwapa kipaumbele wasanii wachanga kuliko wakongwe kinawafanya wasanii
hao wachukuliwe poa.
Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Television Jumatatu hii, Mr Blue amesema kitendo hicho kinawavunja moyo wasanii wengi wakubwa hali ambayo inawafanya wasanii hao kukata tamaa.
“Sio tu wasanii wakubwa hawafanyi vizuri, lakini wanapewa heshima inayostahili kwenye game?,” aliuliza Mr Blue. “Unakuta msanii ndogo ana nyimbo mbili lakini analipwa pesa nyingi kuliko msanii mkongwe, vitu kama hivi vinavunja moyo,”
Rapper huyo amewataka wadau mbalimbali wa muziki nchini kuwapa heshima wasanii wakongwe kwani kufanyahivyo ni kuijenga tasnia ya muziki.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment