July 10, 2016

 


Wanawake waislamu nchini Rwanda,wapigwa marufuku wasijifunike nyuso zao.
Hatua hiii imechukuliwa na jumuiya ya waislamu nchini humo iliyofikia uamuzi wa kuipiga marufuku vazi hilo la Niqab linalovaliwa na wanawake.
Vazi hilo hufunika uso wote wa mwanamke.
Jumuiya hiyo imesema marufuku hiyo inatokana na sababu za kiusalam' Hili vazi ni la kiislamu hata hivyo limeanza kutumika vibaya kwa madhumuni ya kudhuru usalama wa waisilamu na vitendo vinavyokinzana na mafunzi ya dini ya Kiislamu''
''Jambo la pili ni usalama wa nchi. kwa sababu watu wanajificha na kutenda vitendo pasi na kutaka kuonekana''.
''Tumeona fikira potofu tayari ikifuja na ndiposa tukachukua uamuzi huu kuzuia kuenea kwa uovu'' alisema sheikh Mussa Sindayigaya.
Uamuzi huo umetokea wakati kundi la watu 17 wa kiislam wanazuiliwa nchini humo kwa tuhuma za kutaka kujiunga na kundi la IS na kufundisha itikadi za kundi hilo.
Katika msikiti mkuu wa Nyamirambo jijini Kigali ni wakati wa swala ya adhuhuri,,,waislam wengi wanaingia msikitini …lakini huwezi kuona hata mmoja anayevaa niqab miongoni mwa wanawake au mabinti wanaoingia hapa msikitini 

Wanawoiunga mkono kauli hiyo ya jumuiya ya waislam nchini Rwanda wanasema kuwa Niqab ilikuwa imeanza kutumika kuficha maoavu mengi katika jamii.
Aidha wanasema kuwa wanawake waislamu wanapaswa kuwajibika kwa kujiepusha na maovu ambayo sasa yameanza kuchipuka kwa kisingizio cha Niqab.
Kuna wengine walioghadhabishwa na uamuzi huo lakini hawakutaka kuzungumzia suala hilo wakisema wanahofia usalama wao.
Hapo nyuma kundi la waislam zaidi ya 17 lilishikwa na kufunguliwa mashtaka ya kusajili vijana wa kujiunga na kundi la Islamic State na pia kueneza itikadi za kundi hilo.
a kwa waislamu na vilevile warwanda.

Related Posts:

  • Audio: Sumaye akijitoa CCM na kujiunga na UKAWA   August 22 Itabaki katika Historia ya  Tanzania kufuatia waziri mkuu mstaafu wa Awamu ya tatu   Frederick Turuwai Sumaye kujiengua katika chama tawala cha Tanzania CCM na kujiunga na Umoja Wa Katiba … Read More
  • Uzinduzi wa Kampeni za CCM Dar ni shiddahhh!!!!! Umati wa wanachama wa CCM wakiwa katika mkutano huo.   Screen kubwa iliyofungwa jukwaani kwa ajili ya kutoa matukio live kwa walio mbali. Ben… Read More
  • Mgombea Ubunge CHADEMA) arejea rasmi CCM   Mgombea ubunge wa Sikonge kupitia CHADEMA amerejea CCM leo ktk viwanja vya Jangwani DSM. Kumbuka Nkumba alijiunga na CHADEMA baada ya kushindwa kwenye kura za maoni CCM. Alipewa kuipeperusha bendera ya CHADEMA kwe… Read More
  • Magazetini leo 23/august/2015 Jumapili August 23 2015 nachukua time hii kukuunganisha tena na stori kwenye Magazeti ya Tanzania, stori kubwa kwenye Hardnews, Dini na Michezo unaweza kuzipitia hapa kwenye kurasa za mbele na za nyuma kama tulivyotoa … Read More
  • Diamond, Ali Kiba ndani ya jukwaa moja Wasanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Saleh Kiba ‘Aki Kiba’ kesho Jumapili wanatarajiwa kutumbuiza katika uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli. Diamond na Ali Ki… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE