August 31, 2016


 Aliyekuwa mfalme wa taarab Mzee Yussuf amepaa kwenda Makka kuhiji. Mzee Yussuf ambaye kwa sasa anapenda ajulikane kama ‘Ustadh’ badala ya ‘Mfalme’ amepaa na ndege ya Emirates mchana huu. Ustadh Mzee Yussuf ambaye hivi karibuni alitangaza kuachana na muziki wa kidunia, amesisitiza kuwa uamuzi wake huo hautabadilika kamwe. Saluti5 iliyokuwepo uwanja wa ndege - Julius Nyerere International Airport, jijini Dar es Salaam, ilishuhudia watu wengi waliokuwa wakisindikiza ndugu zao wakihamasika na kumpongeza Mzee Yussuf kwa uamuzi wake wa kwenda Hijja
 Mzee Yussuf akiagana na mkewe Leyla Rashid 



Baba mzazi wa Mzee Yussuf naye alikuwepo kumuaga mwanaye

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE