August 14, 2016

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete leo ametoa tamko la Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola  la Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika tarehe 11 Agosti, 2016 kuchagua Rais, Wabunge, Mameya, Madiwani na Kura ya Maoni ya Katiba. 

Rais Mstaafu Kikwete yuko nchini Zambia kufuatia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kumteua kuwa Mwenyekiti wa Timu hiyo yenye waangalizi wa kimataifa 17 kutoka nchi za Jumuiya ya Madola.

Kwa mujibu wa tamko hilo, Jumuiya ya Madola imejiridhisha kuwa zoezi la upigaji kura, usimamizi wa kura na uhesabuji kura vituoni kwa ajili ya umeendeshwa kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni bora za uendeshaji wa chaguzi.

 Tamko linasema, dosari na hitilafu zilizojitokeza hazikuwa kubwa kiasi cha kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu huo.

Amewapongeza wananchi wa Zambia kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa amani na kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka. 

Amewasihi viongozi wa kisiasa wa Zambia, wagombea na vyama vya siasa kuheshimu maamuzi wa wananchi na pale inapojitokeza upande wowote kutoridhika na matokeo, zitumike njia za amani na kisheria za kutafuta ufumbuzi.

Related Posts:

  • CUF kususia maadhimisho ya mapinduzi Chama cha Wananchi kimesema hakitashiriki maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi visiwani Zanzibar kutokana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi. Chama hicho kupitia taarifa kimesema maadhimisho hayo yatafanyika “Serikali ik… Read More
  • Magazeti ya leo January 1 -2016 haya hapa Leo January1 2016, tukiwa tunasherehekea siku ya mwaka mpya, tunakuletea kilichoandikwa katika magazeti ya leo japo kwa ufupi … Read More
  • Wachunguzi waanza kuchunguza chanzo cha motoMaafisa wanasema moto ulianza ghorofa ya 20 upande wa nje na haukusambaa ndani ya hoteli Wachunguzi mjini Dubai wanajaribu kubaini chanzo cha moto uliozuka katika hoteli ya kifahari mkesha wa Mwaka Mpya na kujeruhi watu kadha… Read More
  • Vigodoro, baikoko marufuku BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeanza kung’ata kwa kutumia kanuni ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kelele na mitetemo. Kwa sasa mtu akitaka kufanya sherehe mtaani, kupiga muziki k… Read More
  • KATY PERRY TO JOHN MAYER YOU MAKE ME FEEL LIKE A NATURAL WOMAN   John Mayer and Katy Perry partied like 18-year-old's ... clubbing till 4:30 AM Thursday, and that's after John raged on stage at a concert earlier in the day with the Grateful Dead. Check out the cli… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE