Taarifa kutoka nchini Swaziland zinaeleza kuwa, Rais Zuma ataalikwa katika sherehe za mwaka huu ili na yeye aweza kuonja matunda mazuri ya nchi hiyo. Viongozi hao wawili wamekua na tabia zinazoendana ambapo wamekuwa wakioa wake mara kwa mara. Mswati ana wake 15 na Rais Zuma ana wake 4 akiwa ameoa mara 6.
King Mswati III amesema kuwa sherehe za mwaka huu zitakuwa kubwa sana kwani amealika wakuu wa nchi nyingine na Rais Zuma akiwa mmoja wao.
Hakuna taarifa zilizothibitishwa kutoka kwa watu wa karibu wa Rais Zuma lakini licha ya kuwa tayari ana wake wanne, Rais Zuma amekuwa akisikika kuwa anataka kuoa mke wa tano. Na inaelezwa kuwa desturi katika kabila la wa-Zulu, mwanaume anayeoa wake wengi, mara nyingi huoa mke wa mwisho akiwa mzee na mke huyo huwa ni binti ili kumsaidia.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment