August 29, 2016

yanga_logo_med_hr

Mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Yanga SC na JKT Ruvu uliokuwa ufanyike Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam umeahirishwa.
Mchezo huo uliopangwa kuchezwa Jumatano ya Agosti 31 sasa utapangiwa tarehe nyingine. Na hatua hyo inatokana na Yanga kuomba uahirishwe kwa sababu ina wachezaji wengi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Wachezaji hao ni pamoja na Kipa Deogratius Munishi ‘Dida’, mabeki Vincent Andrew ‘Dante’, Kelvin Yondani na Mwinyi Hajji, kiungo Juma Mahadhi na mshambuliaji Simon Msuva.
Aidha, Yanga pia imesema wachezaji wake wengine, beki Vincent Bossou (Togo), kiungo Haruna Niyonzima (Rwanda) na mshambuliaji Amissi Tambwe (Burundi) nao pia wameitwa na timu zao za taifa na kufanya idadi ya wachezaji wanane kutokuwepo siku hiyo.
Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinaruhusu timu ambayo wachezaji wake wasiopungua watano wameitwa timu za taifa kuahirishiwa mechi.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ameita wachezaji 20 watakaosafiri kwenda Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba ya mechi za Kundi G kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2017).
Mbali na Dida, Yondani, Dante, Mngwali, Mahadhi  na Msuva wengine ni Aishi Manula, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe (Azam FC) na David Mwantika (Azam FC). Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Shiza Kichuya (Simba SC), Ibrahim Jeba (Mtibwa Sugar), Jonas Mkude (Simba SC), Muzamil Yassin (Simba SC), na Farid Mussa (Teneriffe ya Hispania). Washambuliaji ni Jamal Mnyate (Simba SC), Ibrahim Hajib (Simba SC), John Bocco (Azam FC) na Mbwana Samatta – CK Genk ya Ubelgiji.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE