Na Baraka Mbolembole
Yanga inaweza kuishi bila Manji hata kama atakumbukwa, ila Manji hawezi kuishi bila Yanga na ataikumbuka. Amekuwa mtu ambaye hataki wengine wahoji, waseme katika mtindo wa kupinga maamuzi yake.
Sijui amekumbwa na nini kwa maana alikuwa na miaka minne salama na ya mafanikio klabuni hapo.
Ameshinda mataji matu ya Ngao ya Jamii, mengine matatu ya VPL, Moja la
FA Cup huku timu yake ikiwa 8 bora ya Caf Confeder n Cup 2016, ameshinda
pia Cecafa Kagame Cup-klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati mara moja.
Haya ni mafanikio makubwa, tena kwa mtu ambaye hakuwahi kuwa kiongozi wa taasisi kubwa na yenye presha siku zote na akiwa hajawahi kucheza soka,
Manji ni kiongozi ambaye atakumbukwa klabuni hapo. Ametumia pesa nyingi lakini kamwe ataendelea kukumbukwa pia kwa mabaya yake.
Kuwafuta uanachama baadhi ya wanachama wa klabu ambao pengine amewakuta klabuni hapo, zaidi ni kuiangusha ghafla timu ambayo tayari imepiga hatua kubwa ndani ya uwanja. Yanga itaanguka tu ikiwa uamuzi wa Manji utakuwa rasmi.
Ni nani atakaye walipa na kuwafanya nyota wa timu kuendelea kuwa na furaha. Ni nani anaweza kuwa kiongozi-rafiki mzuri wa kocha Hans Van der Pluijm?
Naliona anguko la Yanga bila Manji lakini nitaendelea kuwasapoti wazee majasiri kama Akilimali ambao wana uwezo wa kupinga kwa hoja.
Na Manji akawashinde katika hoja ila asiondoke kwa sababu ya kushindwa kwa mawazo yake. Yeye ni mwenyekiti wa klabu. Amevunja mikataba mingi aliyosema haina maslai.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment