Hakainde Hichilema anaongoza dhidi ya mpinzani wake rais wa sasa Edgar lungu kwa kura zaidi ya elfu sita
Matokeo ya awali ya
uchaguzi wa urais nchini Zambia yanaonyesha kuwa mgombea wa chama
kikuu cha upinzani, Hakainde Hichilema anaongoza kwa ushindi wa kura
chache.
Takwimu za Tume ya uchaguzi zinaonyesha Bw Hichilema yuko
mpele ya Edgar Lungu rais wa sasa wa zambia kwa kura zaidi ya elfu
sita. Tume ya Uchaguzi ya Zambia ilipinga shutuma kutoka kwa Bw Hichilema kwamba ilikula njama na serikali ya kuchelewesha kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Ilisema ushiriki wa wapiga kura zaidi ya asilimia hamsina na saba unamaanisha kwamba shughuli ya kuhesabu kura itachukua muda kuliko ilivyo tarajiwa.
Edgar Lungu alichaguliwa mwaka jana kwa ushindi mdogo kufuatia kifo cha rais aliekuwepo mamlakani wakati huo, Michael Sata
0 MAONI YAKO:
Post a Comment