Kumbukumbu
Na.Baraka Mbolembole
MMOJA wa marefa mwenye ujuzi mkubwa akiwa na miaka 51 sasa, ni Mtaliano pekee aliyekuwa na uwezo wa kuchezesha mechi ngumu bila wasiwasi. Hapa alikutana na maswali kutoka.....
#Swali: Ulisema kwamba dhumuni lako ni kuwa mwenyekiti wa marefa Ulaya? Kwa namna hiyo unazungumzia vipi tukio la Thierry Henrry la kunawa mpira miezi 18 iliyopita pale Ufaransa ilipocheza na Ireland?
#Collina: Nimesema kazi yangu sio kufafanua maamuzi kama hayo ila kuhakikisha makosa yanapungua uwanjani.
#Swali: Ukiwa kama mwamuzi rasmi nini unatakiwa kufanya unapokuwa na mchezo wa UEFA? Na vigezo vipi uwe navyo ili kufanya kazi na UEFA?
#COLLINA: Kikubwa wanaangalia maamuzi yako ya mechi zilizopita, pia utambue sheria na ujue kuzitumia katika maamuzi sahihi, pia refa wa miaka hii ni vizuri uwe na mbio kama mwanariadha sababu michezo ya miaka hii ina spidi sio kama zamani.
Kama utachoka mapema ni dhahiri mechi itakushinda na itakuwa na makosa mengi! Pia lazima ufahamu mbinu mbalimbali za wachezaji ili utoe maamuzi sahihi katika matukio ya dharura. Ila kubwa zaidi ni kutambua timu zinacheza vipi ili uwe na uwezo wa kutabiri njia wanazotumia.
Mfano timu ikitumia 4-3-3 aina ya mchezo utakuwa tofauti na timu inayotumia mfumo wa 4-3-1-2 na utagundua kwamba timu inayotumia mfumo wa kwanza hushambulia kutokea nje ya 18 lakini mfumo wa pili timu husika hukaa sana na mpira na itafunga uwanja kutokea kati mwa uwanja.
Pia ni vyema ukamtambua mchezaji mmoja mmoja kwa sababu wachezaji wana sifa tofauti.
#Swali: Kuwa na maandalizi ya kutosha kutapelekea kuwa na nafasi nzuri ya kutoa maamuzi?
#Collina: Ndiyo ngoja nikupe mfano mwingine wa mechi ya kombe la shirikisho mwaka 2009 kati ya Hispania na Marekani, Hispania walitawala mpira kwa kupanua uwanja kuliko Marekani ambao walikuwa wakitumia mipira mirefu.
Kwa mechi kama hii refa ni lazima upunguze uwanja usiwe mbali na matukio ili uweze kwenda sawa na umudu mchezo.
#Swali: Dhahiri umeshuhudia mechi nyingi, lakini muhimu ni vipi kuangalia 'live' uwanjani au kuangalia kwenye TV?
#COLLINA: Unapoangalia mechi kwenye Tv kuna vitu ambavyo huvioni ukiangalia 'live' uwanjani na unapoangalia 'live' uwanjani kuna pia kuna vitu ambavyo huvioni ukiangalia kwenye Tv.
Ninapoangalia mechi nyumbani naweza kuangalia mechi sita kwa siku ila ninapoangalia 'live' uwanjani huwa naangalia mechi mbili tu kwa siku. Kwa mwamuzi ni vizuri akiangalia mechi 'live' uwanjani kwa sababu kuna matukio ambayo kamera haionyeshi, hii humsaidia mwamuzi kupata faida zaidi.
#Swali: Ukiwa kama mwamuzi una mtazamo gani mwingine kuhusiana na masuala ya kiufundi?
#Collina: Kuna bodi ya soka ya Kimataifa ambayo wanaamua na wanatumia teknolojia mpya ya maamuzi kila siku na sio mimi. Kazi yangu mimi ni kuzifanyia na kutendea haki zile sheria/teknolojia zilizotungwa na wao.
Katika Ligi ya Ulaya na Ligi ya Mabingwa kuna waamuzi wawili wameongezwa wa ziada kwa madhumuni ya kupunguza baadhi ya matukio ya utata na kutoa maamuzi yanayoridhisha, hivyo pia Uefa wamepitisha sheria hii kwenye mashindano ya Ulaya yatakayofanyika Ukraine na Poland mwaka 2012.
#Swali: Unazungumziaje soka la Italia kwa sasa?
#Collina: Muda mwingine Italia mashabiki wanashindwa kufahamu kuwa matokeo tofauti ni sehemu ya mchezo, mfano ni mechi kati ya CF Cologne na Bayern Munich ambayo hadi halftime Bayern walikuwa wakiongoza 2-0 lakini mwisho mechi iliisha kwa Cologne kushinda 3-2, au mechi ya Arsenal na Newcastle ambayo kabla ya halftime Arsenal walikuwa wakiongoza mabao 4-0 lakini mwisho mechi iliisha kwa sare ya mabao 4-4.
Italia inapaswa watambue sasa mpira umebadilika timu yoyote inaweza kufungwa kwenye mchezo. Na jambo lingine kuwa wapenzi na wachambuzi wa soka wanachambua mabaya tu ya waamuzi na si mazuri hili ni tatizo pia.
#Swali: Unafikiria ni kitu gani kinadumaza soka la Italia?
#Collina: Sina uhakika sana, ila soka la Italia bado lipo kwenye chati sema uwepo wa wageni wengi katika timu kubwa za Italia kunapelekea kuzorotesha kiwango cha timu ya taifa ya Italia.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment