September 01, 2016


15

Mmiliki wa Facebook, Mark Zuckerbag yupo barani Afrika ambapo anafanya ziara kujionea maendeleo ya teknolojia katika baadhi ya nchi.
Mark Zuckerbag aliitembelea Nigeria ambapo alijionea namna mtandao wa Facebook unavyofanya kazi na kuweza kuwaunganisha watu mbalimbali. Baada ya kumaliza ziara yake nchini Nigeria, Mark aaliwasili nchini ya Kenya Jumatano Agosti 31.

16
Akiwa nchini Kenya ametembelea kituo kimoja cha iHub ambacho kimetengeneza mfumo unaowezesha wateja wa mitandao ya simu kununua gesi ya nyumbani kwa kitumia simu zao.
Kingine kikubwa kilichozua gumzo ni baada ya bilionea huyo kuingia katika mgahawa mmoja jijini Nairobi akiwa na Waziri wa Habari wa Kenya na kuonekana akila Ugali, Sukuma wiki na Samaki.

15 

Mark alitembelea mgahawa wa Mama Oliech ambapo aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa kila akitembelea taifa lolote, hupenda kujaribu chakula wanachotumia, na kuwa aliupenda sana Ugali na Samaki ikiwa ni mara yake ya kwanza kula chakula hicho.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE