Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amejiuzulu nafasi yake ya ubunge na kupisha uchaguzi mdogo katika jimbo lake la Witney.
Cameron ambaye alijiuzulu nafasi
yake ya Waziri Mkuu wa Uingereza Juni mwaka huu baada ya kupigwa kwa
kura ya Uingereza kujitoa ndani ya Muungano wa Ulaya (EU) amesema kuwa
hatiki kuwa kikwazo kwa Waziri Mkuu wa sasa, Theresa May.
Cameron amekuwa Mbunge wajimbo la
Witney tangu mwaka 2001. Alisema kuwa ni furaha kubwa kulitumikia jimbo
hilo kwa miaka yote hiyo lakini itakuwa ni vigumu kwake kuendela kuwa
mbunge bila kuwa kikwazo katika shughuli serikali.
Aidha, alieleza kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo alimuelewa pindi alipomwambia kuhusu uamuzi huo wa kujiuzulu
0 MAONI YAKO:
Post a Comment