October 31, 2016



Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kukata rufaa kwa njia ya mtandao ikiwa hawajaridhsihwa na matokeo ya upangaji uliotangazwa hivi karibuni.

Serikali imetenga Tshs 483 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa jumla wanafunzi 119,012 – kati yao, wanafunzi 93,295 ni wanaondelea na masomo na wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi 20,183 wa mwaka wa kwanza wameshapata mikopo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao (Online Loan Application and Management System) kuanzia leo (Oktoba 31, 2016) hadi Januari 31, 2017.

“Wanachotakiwa kufanya wanafunzi ni kuingia katika mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa Afisa Mikopo wa chuo chake ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo chake kwa barua kwa ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” amesema Bw. Badru.

ANGALIZO: Ada ya Maombi ya Tshs 10,000/- iliyopaswa kulipwa na waombaji mikopo kwa MPesa kwa ajili ya malipo ya Rufaa (HESLB) imefutwa.Taratibu nyingine zinabaki palepale

Related Posts:

  • New Audio: Ally Kiba - Chekecha cheketua Baada ya kufanya poa ndani na nje ya Tanzania na wimbo wake wa mwana, Mwanamuziki Ally Kiba sasa amekuja na ngoma yake mpya kabisa inayoitwa Chekecha cheketua. … Read More
  • Rais Kikwete afanya uteuzi mpya    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) atika uteuzi huo, Rais amemteua Mhe… Read More
  • Di Maria ajuta kujiunga na Man United    Mchezaji nyota ambaye pia ni kiungo wa kati wa Manchester United Angel Di Maria amesema kuwa alifanya makosa kujiunga na Kilabu ya Manchester United msimu uliopita. Raia huyo wa Argentina amejaribu kuingian… Read More
  • Tp Mazembe yasajili watatu    Kikosi cha TP Mazembe cha Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo  Timu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo imewasajili wachezaji watatu wapya toka kwenye timu ya taifa ya Ivory Coast. Nyota … Read More
  • Waliomuiba Albino Pendo Wakamatwa Mwanza   Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amesema watu wote waliohusika ‘kuiba’ mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (albino) Pendo Emmanuel (4) katika kijiji cha Ndami wilayani Kwimba, Mwanza, wamekamatwa. … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE