Madereva na wasidizi wa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mbalimbali
waolikuwa tayari wameshafika mkoani Simiyu kwaajili ya kusherehekea
kilele cha mbio za mwenge, wameeleza kuumizwa na agizo la Rais John
Magufuli la kurejesha fedha za kujikimu.
Baadhi wamesema kuwa hawana uwezo wa kuzirejesha fedha hizo kwani
hawakuwaomba kufanya safari hizo kwakuwa ilikuwa sehemu ya kazi zao
kwahiyo kiasi cha fedha hizo walizitumia kama walivyokubaliwa na ofisi
kuwawezesha na kufika katika eneo hilo.
“Sisi hatukuomba kuja Bariadi kwenye sherehe za mbio za Mwenge wa
uhuru, tuliambiwa kuja na tukapewa fedha ambazo tumezitumia kwa mujibu
wa mahesabu ya matumizi tuliyoandikiwa kwasababu ilibidi tule na kulala
kwenye nyumba za wageni,tutapata wapi hela za kuzirudisha, hapo sisi
kosa letu liko wapi,”? alihoji mmoja wa madereva aliliambia gazeti la
The Citizen.
“Ili nibidi nilipe chumba kwa siku 7 ambazo nilitarajia kuishi hapa
kama nilivyotumwa kwa uhaba wa vyumba,sasa naanzaje kumwambia mmenyewe
arudishe fedha yote ili niirejeshe ofisini ?alihoji.
Wiki iliyopita Rais John Magufuli alisitisha safari ya viongozi wa
mikoa na wilaya kwenda Simiyu kwenye kilele cha mbio za Mwenge na
kuwataka wale waliokwisha chukua posho kuzirejesha.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment