Tanzania
imeanza kuandaa kikosi kipya cha timu ya taifa ya vijana wenye umri wa
chini ya miaka 17 – Serengeti Boys kitakachoshindana kuwania Kombe la
Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka hiyo.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), limeiteua Tanzania kuandaa
fainali hizo mwaka 2019 hivyo sasa TFF imeanza kuandaa vijana wake.
Kwa kuanzia tu, imeanza kuwamuisha vijana 22 wanaosoma Shule za Alliance zilizoko Mwanza.
Mapema
wiki hii, ilimuagiza Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu kwa
Vijana, Kim Poulsen kupima uwezo wa vijana hao kwa kufanya nao mazoezi
kwenye viwanja vya Alliance ambako amemaliza leo asubuhi na kusema:
“Tuna timu bora ya taifa.”
“2019
si tu kwamba Tanzania itashiriki, bali kushindana. Lakini naipongeza
TFF na Alliance kwa kuanza program ya kuandaa timu bora. Serengeti Boys
ya sasa inayomaliza muda wake iliandaliwa kwa mwaka mkoja, lakini vijana
hawa wenye umri wa miaka 12 na 13 ni hazina nyingine kubwa kwa taifa.
“Kwa
jinsi nilivyowaona itoshe kusema tu tayari tuna timu. Nimesikia
viongozi wa TFF wakisema kwamba jicho lao si kwa vijana hawa tu, bali
pia kwa vijana wengine Tanzania nzima. Hili ni jambo zuri lenye manufaa
mazuri,” amesema Poulsen alipozungumza na waandishi wa habari leo mara
baada ya mazoezi ya asubuhi.
Nahodha
wa timu hiyo ya vijana, alishukuru Alliance kwa malezi mazuri na TFF
kwa kuendelea kuwajali hasa kwa sasa ambako nao wamesema ndoto zao ni
kutaka kung’ara zaidi ya Serengeti ya sasa ambao walitolewa na Congo
Brazzaville katika harakati za kuwania nafasi ya kushiriki fainali za
Kombe la Mataifa Afrika, zitakazofanyika mwakani nchini Madagascar.
Vijana
waliotolewa kwa sasa wanajipanga upya kwenda Korea Kusini kwa ajili ya
kujiandaa na ratiba mpya ya CAF na FIFA kwa vijana wenye umri wa chini
ya miaka 20 ambako timu ya taifa kwa hapa Tanzania inaitwa Ngorongoro
Heroes. Ratiba za michuano ijayo ya kimataifa, itatolewa baadaye mwaka
huu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment