Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli
amewataka watanzania kumuenzi kwa vitendo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere kwa kuwahudumia Wazee nchini kwa kuwapatia
mahitaji ya muhimu kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.
Akiongea
na Wazee katika Kambi ya kulea wazee ya Chazi iliyopo Wilayani Mvomero
Mkoani Morogoro Mama Janeth amesema kuwa watanzania wanapaswa kutambua
Wazee ni kundi muhimu kwa ustawi wa nchi kwani miongoni mwao walishiriki
katika ukombozi wa taifa leo hivyo tuitumie Siku kama ya leo na
nyingine kumuenzi Hayati mwalimu Julius Nyerere akiwa kama mzee
aliyetangulia mbele za haki.
“Leo
ni siku muhimu sana katika taifa letu siku ambayo tunaenzi siku
aliyofariki muasisi awa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere, hivyo ni rai yangu kwa watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa
kushiriki kwa pamoja katika kuwahudumia wazee na kuwapatia mahitaji yao
muhimu” Alisema Mama Janeth.
Aidha,
Mama Janeth alisema kuwa amesikia changamoto zinazokabili Makazi hayo
na ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau kwa kadri iwezekanavyo ili
kuhakikisha wanapunguza na kuondoa kabisa changamoto hizo iwe makazi ya
wazee Chazi na yote nchini yawe sehemu salama ya kuwahudumia wazee.
Katika
kutembelea kituo hicho Mamam Janeth Magufuli ametoa zawadi ya mchele,
Maharagwe,unga na mafuta ya kupikia kwa ajili ya wazee na watu
wasiojiwezakatika kituo hicho.
Akimkaribisha
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema kuwa
serikali ya mkoa wake inatekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. john Pombe Magufuli ya kuwahudumia wazee
na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani mkoa wameshaanza kutatua
baadhi ya kero na wataendelea kufanya hivyo ili kuyaimarisha makazi ya
wazee mkoani humo.
Pia
Dkt. Kebwe amewataka watu wote waliovamia makazi ya wazee kuondoka mara
moja na kutafuta maeneo mengine na atakayekiuka agizo hilo serikali
itamchukulia hatua kali za kisheria.
Akiwasilisha
Risala ya Makazi ya Ya wazee ya Chazi kwa Mama Janeth Magufuli Kaimu
Afisa Mfawidhi wa Makazi hayo Bw. Richard Kamwana amemshukuru Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa misaada
aliyoitoa kwa wazee wa kituo hicho wakati wa sikukuu ya Eid.
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kiombo
amemuhakikishia Mama Janeth Magufuli wataendelea kushirikiana na taasisi
nyingine katika kukiendeleza kituo hicho ikiwamo kuwapatia wazee wote
kadi za CHF kwa ajili ya kuwasaidia wazee hao kupata huduma ya Afya
popote waendapo.
Na Hassan Silayo-MAELEZO
0 MAONI YAKO:
Post a Comment