
Akizungumza katika viwanja vya mahakama hiyo mwanasheria wa CHADEMA Mh John Malya amesema katika kesi hiyo wamewashtaki watu wanne akiwemo Meya wa manispa hiyo Benjamin Sitta na msimamizi wa uchaguzi.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kinondoni Mh Mustapaha Muro na ambaye ni moja ya walalamikji katika kesi hiyo akiwa kama ni mgombea wa nafasi ya umeya amesema wamekimbilia mahakamani ili kupata haki yao.
Henry Kileo ni katibu wa chama hicho mkoa wa Kinondoni ambaye anawataka wananchi kuwa watulivu wakati suala hilo lipo mahakamani na waamini kuwa haki itatendeka tuu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment