
Mshindi wa miss Tanzania 2016/2017 Diana Edward Lukumai kutoka Kinondoni
Usiku
wa kuamkia Jumapili ya Oktoba, 30 jijini Mwanza kumefanyika mashindano
ya Miss Tanzania 2016 ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu serikali
ilipotangaza kuyafungua mashindano hayo Disemba, 2014.
Katika
mashindano ya mwaka huu kama kawaida ya mashindano hayo
walimbwende walipanda jukwaani na kuonyesha uwezo wao wa kutembelea kama
ma’miss’ lakini pia uwezo wa kujibu maswali ambayo yaliandaliwa na
majaji.
Baada ya mchakoto wote kukamilika,
mwanadada Miss Kinondoni 2016, Diana Edward alitangazwa kuwa mshindi
wa Miss Tanzania kwa mwaka 2016, nafasi ya pili ikishikiliwa na Maria
Peter na mshindi wa tatu akiwa ni Grace Malikita.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment