Obama: 'Ninamuunga mkono' Donald Trump
Rais mteule wa Marekani Donald Trump
amesema kuwa ni ''heshima'' kubwa kukutana na rais Barrack Obama katika
mazungumzo ya mpito yaliofanyika katika ikulu ya White House.
Bwana Obama amesema kuwa ametiwa moyo kuhusu mazungumzo yao ya maswala mbalimbali yaliochukua zaidi ya saa moja.Bwana Trump ametilia shaka uraia wa rais Obama na kuapa kuharibu ufanisi wake wakati wa utawala wake.
Wakati wa kampeni bwana Obama alisema kuwa bwana Trump 'hafai' kuongoza Marekani.
Hatahivyo Obama alisema kuwa ''anamuunga'' mkono baada ya kumshinda Hillary Clinton.
Baada ya mkutano huo wa ikulu rais Obama alisema kuwa kipaombele chake sasa katika miezi miwili ijayo ni kuhakikisha kuwa kundi litakalosimamia shughuli za mpito linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa wamezungumza sera za nyumbani pamoja na zile za kigeni na kwamba amefurahishwa na maoni ya Donald Trump kwamba yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika maswala yanayokabili Marekani.
Bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika siku zijazo.

Trump awasili White House
Waandishi wa habari wakimsubiri Trump White House
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amewasili katika Ikulu ya White House, kwa mujibu wa maafisa nchini Marekani.
Hata hivyo aliingia akitumia mlango tofauti na kuwasili kwake hakukunaswana kamera za waandishi wa habari.Anatarajiwa kuwa kwenye mazungumzo na Rais Obama wakati huu.
Licha ya tofauti zao, bwana Obama siku ya Jumatano alikishauri kikosi chake kufanya jitihada zaidi kuhakisha kuwa kuna mafanikio kwenye shughuli ya kupokeza madaraka kwa Republican mwezi Januari.
Mapema kikosi cha kampeni ya Trump kilikutana na washauri kujadili masuala kuhusu siku za kwanza 100 za Trump kama rais na uteuzi muhimu katika nyadhifa za serikali.
Majina yaliyotajwa ni kati ya wale waliomuunga mkono Trump kutoka mwanzo akiwemo aliyekuwa spika Newt Gingrich, maseneta Jeff Sessions na Bob Corker pamoja na aliyekuwa meya wa New York Rudy Giuliani.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment